Home Michezo Kipyegon atuzwa bora ulimwenguni

Kipyegon atuzwa bora ulimwenguni

0

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Faith Kipyegon,alitawazwa mwanariadha bora wa mwaka katika mashindano ya uwanjani .

Kipyegon alikuwa na mwaka wa kufana akivun ja rekodi tatu za dunia ya mita 1500,mita 5,000 na maili moja kando kuhifadhi taji ya dunia mjini Budapest.

Kipyegon alikuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kushinda tuzo hiyo.

Mshikilizi wa rekodi ya marathon Kelvin Kiptum alipokea tuzo ya mwanariadha bora katika mashindano ya nje ya uwanjani, huku Faith Cherotich na Emmanuel Wanyonyi wakitwaa tuzo za chipukizi bora wa mwaka.

Wakenya hao wanne walikuwa Monaco kupokea tuzo zao Jumatatu usiku.

Website | + posts