Home Michezo Kipyegon aorodheshwa kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka kwa vidosho

Kipyegon aorodheshwa kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka kwa vidosho

0
Faith Kipyegon

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon ameteuliwa katika orodha ya mwisho ya wanariadha watano wanaowania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka huu kwa wanawake.

Kipyegon ameteuliwa baada ya kushinda dhahabu mbili za dunia mwaka huu katika mbio za mita 1,500 na 5,000 na kuweka rekodi mpya za dunia za mita 1,500, 5,000 na maili moja.

Waaniaji tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka huu

Wengine wanaowania tuzo huyo ni mabingwa wa dunia Yulimar Rojas wa Venezuela, Shericka Jackson wa Jamaica, Femke Bol wa Uholanzi na bingwa wa Berlin Marathon Tigist Asefa kutoka Ethiopia.

Mshindi atabainika katika hafla itakayoandaliwa mjini Monaco, Ufaransa Disemba 11 mwaka huu.

Kipyegon anawania kuwa mwanamke wa kwanza wa Kenya kutwaa tuzo hiyo.

Website | + posts