Home Kimataifa Kipyegon ahifadhi taji ya Olimpiki kwa mara ya pili

Kipyegon ahifadhi taji ya Olimpiki kwa mara ya pili

0
kra

Faith Kipyegon ndiye bingwa mpya wa Olimpiki, akiwa mwanariadha wa kwanza kushinda dhahabu tatu za Olimpiki katika mita 1,500 .

Kipyegon ametwaa dhahahbu katika fainali ya Jumamosi usiku akitimka kwa dakika 3 sekunde 51.29, ikiwa rekodi ya Olimpiki.

kra

Fedha ilimwendea Jessica Hull wa Australia kwa dakika 3 sekunde 52.56, naye Mwingereza George Bell,akiridhia shaba kwa dakika  3 sekunde 52.61.

Kipyegon ambaye pia ni bingwa wa Dunia ameshinda dhahabu na fedha katika makala ya mwaka huu ya michezo ya Olimpiki ya Paris.