Home Michezo Tanzania yalenga viwanja vitatu katika ombi la pamoja la AFCON 2027

Tanzania yalenga viwanja vitatu katika ombi la pamoja la AFCON 2027

Wakaguzi wa CAF wameanza ziara ya kukagua viwanja vya mataifa ya Afrika mashariki kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

0

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF,Wallace Karia ana imani bid ya pamoja ya mataifa ya Afrika mashariki kuandaa kipute cha AFCON mwaka 2027 itafalu.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na KBC, Karia amefichua kuwa wanapania kuwa na viwanja vitatu katika bid yao:- ule wa Benjamin Mkapa-Daresalam,Amani Zanzibar na kiwanja kipya kitakachojengwa mjini Arusha.

“Tayari kiwanja cha Amani Zanzibar tunatarajia kitakuwa tayari kufikia Disemba na Benjamin Mkapa itakuwa tayari mwezi wa 10 kabla, ya kuanza kwa Super League na kiwanja kimoja tunapanga kujenga Arusha kuwa standby”akasema Karia

Kuhusu miundo msingi mingine,Karia amesema Tanzania wanajivunia mikahawa bora,usafiri shwari na pia usalama wa kutosha tayari kwa mashindano hayo.

“Movement ya kwenda viwanjani katika miji yote ifikiapo wakati wa mashindano tuna imani itakuwa vizuri,usalama wetu ni mzuri na tunaimani itakuwa AFCON ya historia na cha muhimu mataifa yote matatu yanaunganishwa na usafiri mzuri wa angani” akaongeza Karia

Karia ambaye pia ni Rais wa shirikisho la CECAFA, ameelezea matumaini makubwa ya ombi hilo la AFCON kufaulu kutokana na ari ya serikali husika za mataifa matatu na pia ari ya usimamizi wa soka .

Wakaguzi wa CAF wameanza ziara ya kukagua viwanja vya mataifa ya Afrika mashariki kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Ivory Coast imetwikwa jukumu la kuandaa fainali za AFCON mwaka 2024 huku CAF ikiwatarajiwa kutangaza mwenyeji wa makala ya mwaka 2025 na 2027.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here