Home Habari Kuu Kiptum na Kipyegon watuzwa wanariadha bora wa mwaka Afrika

Kiptum na Kipyegon watuzwa wanariadha bora wa mwaka Afrika

0

Mshikilizi wa rekodi ya Marathon Kelvin Kiptum  na bingwa mara mbili  wa Olimpiki  katika mbio za mita 1,500  Faith Kipyegon,  ndio wanariadha bora wa mwaka barani Afrika. 

Wawili hao walituzwa na shirikisho  la Riadha barani Afrika baada ya kunawiri, Kiptum  akishinda mbio za London  na Chicago Marathon na kuweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2 na sekunde 35.

Kipyegon alihifadhi taji ya dunia ya mita 1,500,  akaibuka bingwa dunia katika mita 5,000  na kuvunja rekodi za dunia katika mita 1,500,5,000  na maili moja katika kipindi cha mwezi mmoja.

Patrick Sang alitawazwa kocha bora wa mwaka huku Janeth Jepkosgei akinyakua tuzo ya kocha bora anayeibuka.

Emmanuel Wanyonyi  na Faith Cherotich walitawazwa wanariadha chipukizi bora wa mwaka.

Website | + posts