Home Michezo Kiptum alenga kutimka Rotterdam chini ya saa mbili mwaka ujao

Kiptum alenga kutimka Rotterdam chini ya saa mbili mwaka ujao

0

Bingwa wa Chigaco Marathon na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathaon Kelvin Kiptum, amethibitisha kushiriki mbio za Rotterdam marathon April 14 mwaka ujao akinuia kutimka chini ya saa mbili.

Kiptum ambaye pia ni bingwa wa London Marathon mwaka huu, aliwashangaza wengi na hatua hiyo badala ya kutetea taji ya London.

Mwanariadha huyo ambaye alivunja rekodi ya Eliud Kipchoge mwaaka huu, anaamini ana uwezo wa kuandikisha muda wa chini ya saa 2 katika mbio za Rotterdam zinazoaminiwa na wadadisi kuwa na mkondo wenye kasi zaidi.