Home Michezo Kiptoo atwaa ubingwa wa Shanghai Marathon akiweka rekodi mpya

Kiptoo atwaa ubingwa wa Shanghai Marathon akiweka rekodi mpya

0

Mkenya Philimon Kiptoo Kipchumba ameandikisha rekodi mpya ya Makala yam waka huu ya mbio za Shanghai Marathon zilizoandaliwa Jumapili.

Kiptoo ametwaa ubingwa akisajili rekodi mpya ya saa 2 dakika 5 na sekunde 35 akivunja rekodi ya awali ya saa 2 dakika 7 na sekunde 14 iliyoandikishwa mwaka 2015 na Mkenya mwenza Paul Lonyangata.

Alphonce Felix Simbu wa Tanzania amemaliza wa pili kwa saa 2 dakika 5 na sekunde 39 huku Solomon Kirwa Yego wa Kenya akiambulia nafasi ya tatu .

Sally Kipyego wa Kenya alimaliza wa pili katika mbio za wanawake akitumia saa 2 dakika 21 na sekunde 51 nyuma ya mshindi Siranesh Dagne wa Ethiopia aliyetumia saa 2 dakika 21 na sekunde 28 kukata utepe.

Eunice Chebichii Chumba amemaliza wa tatu huku wanariadha 38,000 wakishiriki.

Website | + posts