Abel Kipsang na Reynold Kipkorir ndio wakenya watakaojitosa uwanjani jumatano usiku katika fainali ya mita 1500 mjini Budapest Hungary.
Kipsanga anaorodheshwa wa tatu ulimwenguni huku Kipkorir akishikilia nafasi ya 9 duniani.
Kenya ilinyakua dhahabu ya dunia ya mita 1500 kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2009 kabla Jake Whigtman wa Uingeteza kutwaa ubingwa mwaka uliopita.
Upinzani mkubwa wa wanariaha wa Kenya unatarajiwa kutoka kwa bingwa wa Olimpiki Jakub Ingebrigsten wa Norway.