Home Kimataifa Kipsang: Marufuku dhidi ya mikutano shuleni muhula wa tatu yangalipo

Kipsang: Marufuku dhidi ya mikutano shuleni muhula wa tatu yangalipo

Katibu wa elimu ya msingi Belio Kipsang, alisema agizo lililotolewa Januari 21, 2021, lingalipo.

0
Katibu wa elimu ya msingi Dkt. Belio Kipsang.
kra

Wizara ya elimu imekariri agizo lake la kupiga marufuku shughuli za ziada katika muhula huu wa tatu wa kalenda ya masomo.

Katibu wa elimu ya msingi Belio Kipsang, alisema agizo lililotolewa Januari 21, 2021, lingalipo.

kra

“Mnakumbushwa kuhusu agizo lililotolewa Januari 21, 2021, linalopiga marufuku shughuli na ziara shuleni katika muhula wa tatu,” alisema Kipsang.

Agizo hilo linanuiwa kuwapa wanafunzi muda wa kutosha kwa shughuli za masomo na pia kuondoa uwezekano wowote wa visa vya wizi wa mitihani huku watahiniwa katika shule za upili wakijiandaa kufanya mitihani yao ya mwisho ya kitaifa.

Baadhi ya shughuli ambazo zilipigwa marufuku ni pamoja na mikutano mikuu ya mwaka ya wazazi, sherehe za kutoa zawadi na siku ya maombi katika shule za msingi na sekondari.

Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne ‘KCSE’ unatazamiwa kuanza rasmi mapema mwezi Novemba.

Website | + posts