Home Michezo Kipchoge na Jepchirchir kuongoza Kenya kutetea mataji ya Olimpiki

Kipchoge na Jepchirchir kuongoza Kenya kutetea mataji ya Olimpiki

Timu ya wanawake itaongozwa na bingwa mtetezi Peres Jepchirchir,ambaye alishinda mbio za London marathon mwaka huu akiweka rekodi mpya ya dunia ya wanawake ya saa 2 dakika 16 na sekunde.

0

Mabingwa watetezi Eliud Kipchoge na Peres Jepchirchir, wataongoza Wakenya kutetea mataji ya mbio za marathon katika michezo ya Olimpiki, iliyoratibiwa kuandaliwa jijini Paris Ufaransa kati ya Juai 26 na Agosti 11 nchini Ufaransa.

Kulingana na orodha ya mwisho iliyotangazwa Jumatano na kamati ya Olimpiki Kenya ,Kipchoge ambaye atakuwa akiwania taji ya tatu mtawalia ya Olimpiki atashirikiakana na wenzake Benson Kipruto, aliyeshinda Tokyo marathon mwaka huu,bingwa wa mwaka huu wa London marathon Alexander Mutiso, huku Timothy Kiplagat aliyemaliza wa pili katika mbio za Tokyo akiwa mwanariadha wa akiba.

Eliud Kipchoge akitwaa dhahabu ya Olimpiki mwaka 2020

Timu ya wanawake itaongozwa na bingwa mtetezi Peres Jepchirchir,ambaye alishinda mbio za London marathon mwaka huu akiweka rekodi mpya ya dunia ya wanawake ya saa 2 dakika 16 na sekunde.

Hellen Obiri, ambaye pia alitetea taji ya Boston marathon kando na kushinda mbio za Boston na Chicago marathon mwaka uliopita, atakuwa akishiriki marathon ya Olimpiki kwa mara ya kwanza,baada ya kutwaa fedha za mita 5,000 mwaka 2016 na 2020.

Peres Jepchirchir akishinda dhahabu ya Olimpiki mwaka 2020

Bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei yupo kikosini akipania kuboresha nishani ya fedha aliyonyakua katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo .

Mshindi wa nishanani ya fedha ya London marathon Sharon Lokedi,ameteuliwa kuwa mwanariadha wa akiba.