Mabingwa watetezi Eliud Kipchoge na Peres Jepchirchir ni miongoni mwa wanariadha 20 waliojumuishwa katika kikosi cha awali cha marathon kwa mashindano ya Olimpiki mwaka ujao jijini Paris nchini Ufaransa.
Kulingana na Mkurugenzi wa Mashindano katika chama cha Riadha Kenya Paul Mutwii, wanariadha hao watachujwa hadi watano kwa wanaume na wanawake watano tarehe 3 mwezi ujao na wanariadha wa akiba wawili.
Kikosi cha wanaume kinawajumuisha mshikilizi wa rekodi ya dunia Kelvin Kiptum, Vincent Ngetich, Timothy Kiplagat, Benson Kipruto, Bernard Koech, Geoffrey Kamworor, Cyprian Kotut, Amos Kipruto na Titus Kipruto.
Kikosi cha wanawake kinamjumuisha mshikilizi wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei, bingwa mtetezi Jepchirchir, Ruth Chepngetich, Rosemary Wanjiru, Joycilline Jepkosgei, Sheila Chepkirui, Judith Jeptum Korir, Selly Chepyego, bingwa wa New York City Marathon Hellen Obiri na Sharon Lokedi.