Home Michezo Kipchoge awinda taji ya tano ya Berlin Marathon Jumapili

Kipchoge awinda taji ya tano ya Berlin Marathon Jumapili

0

Makala ya 49 ya mbio za Berlin yataandaliwa Jumapili hii Septemba 24 nchini Ujerumani huku bingwa mtetezi na mshikilizi wa rekodi ya dunia Eliud Kipchoge, akimenyana na Amos KiPruto.

Kipchoge alitwaa ushindi mwaka uliopita kwa mara ya nne, akiweka rekodi mpya ya dunia saa 2 dakika 1 na sekunde 9, na atakuwa akiwinda taji ya tano.

 

Kwa upande wake Kipruto aliye na umri wa miaka 30, anajivunia kumaliza wa pili katika mbio za Tokyo Marathon mwaka uliopita kabla ya kushinda London marathon mwaka uo huo .

Kipruto aliye na muda bora wa saa 2 dakika 3 na sekunde 13, atakuwa anaktana na Kipchoge katika mbio za Berlin baada ya kumaliza wa pili nyuma ya bingwa wa Olimpiki katika makala ya mwaka 2018.

Wakenya wengine watakaotimka mbio za wanaume ni Jonathan Maiyo ,Eliud Kiptanui ,Ronald Korir ,Philemon Kiplimo ,Enock Onchari ,Mark Korir na Josphat Boit .

Sheila Chepkurui ndiye Mkenya pekee katika mbio za wanawake akipambana na bingwa mtetezi Tigist Tufa wa Ethiopia miongoni mwa wengine.

Website | + posts