Home Michezo Kip Keino Classic kuandaliwa Aprili mwaka ujao

Kip Keino Classic kuandaliwa Aprili mwaka ujao

0

Mashindano ya kila mwaka ya Kip Keino Classic Continental Tour yataandaliwa Aprili 20 mwaka ujao.

Kwa kawaida, mkondo wa Kenya umekuwa ukiandaliwa mwezi Mei.

Hata hivyo, kulingana na Mkurugenzi wa mashindano hayo Baranaba Korir, wamelazimika kuyaandaa mwezi Aprili ili kutoa fursa kwa ukarabati wa uwanja wa Kasarani utakaoanza mwezi Mei.

Mashindano ya Kenya ndio ya pekee ya nembo ya dhahabu ambayo yamekuwa yakiandaliwa Afrika.

Website | + posts