Home Kimataifa Kiongozi mkuu wa vita vya Israel amkosoa Netanyahu kuhusu mkakati wa Gaza

Kiongozi mkuu wa vita vya Israel amkosoa Netanyahu kuhusu mkakati wa Gaza

Hamas iliwauwa takriban watu 1,300 na kuchukua mateka 240.

0

Mjumbe mkuu wa baraza la mawaziri la vita la Israel amemshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kutosema ukweli kuhusu malengo ya kijeshi ya nchi hiyo kuhusu Gaza.

Netanyahu amekataa hadharani msukumo wa Marekani wa kutaka kuwepo kwa taifa la Palestina siku zijazo na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yataendelea “hadi ushindi kamili”.

Lakini Gadi Eisenkot – ambaye mtoto wake aliuawa alipokuwa akipigana Gaza – alisema wale wanaotetea “kushindwa kabisa” kwa Hamas “hawasemi ukweli”.

Jenerali huyo mstaafu pia alisema Bw Netanyahu “anawajibika pakubwa na kwa wazi” kwa kushindwa kulinda nchi yake tarehe 7 Oktoba na akahimiza uchaguzi mpya, akisema “hakuna imani” na uongozi wa sasa wa Israeli.

Hamas iliwauwa takriban watu 1,300 na kuchukua mateka 240 katika shambulio lao la kushtukiza kusini mwa Israel.

Mvutano kati ya baraza la mawaziri, kukiwa na ripoti kwamba waziri mkuu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant hawana maelewano mengi, inakuja huku mtafaruku kati ya Israel na washirika wake wa Magharibi ukiongezeka.

Baada ya maoni ya Bw Netanyahu kuhusu utaifa wa Palestina, mshauri wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema Marekani na Israel “zinaona mambo kwa njia tofauti”.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema kuwa hakuna njia ya kutatua changamoto za kiusalama za Israel bila kuwa na taifa la Palestina.