Home Habari Kuu Kiongozi Mkuu wa Hamas auawa nchini Iran

Kiongozi Mkuu wa Hamas auawa nchini Iran

Kifo cha Haniyeh kimejiri saa chache baada ya kushiriki sherehe ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian.

0
Kiongozi mkuu wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh,ameuawa.
kra

Kiongozi mkuu wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh, ameuawa nchini Iran kwa mujibu wa kundi hilo.

Kifo cha Haniyeh kimejiri saa chache baada ya kushiriki sherehe ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian.

kra

Hamas ilisema Haniyeh aliuawa kupitia shambulizi la angani kwenye makazi yake Jijini Tehran.

Wiki kadhaa baada ya shambulizi lililotekelezwa na Hamas Oktoba 7,2023 nchini Israel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema ameagiza shirika la ujasusi nchini humo Mossad, kuwawinda na kuwaangamiza viongozi wa Kundi la Hamas.

Licha ya kuwa Israel inatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, hakuna aliyekiri kuwajibika na kisa hicho.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema waliotekeleza mauaji hayo watakabiliwa vilivyo, akiongeza kuwa Iran italinda maadili na heshima yake.

China, Jordan na Lebanon pia zimekashifu mauaji hayo, zikisema hatua hiyo itazidisha uhamasama katika eneo hilo.

Kwa upande wake Jeshi la  Irani lilisema linachunguza tukio hilo.