Home FKF Premier League Kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Kenya kuingia awamu ya 22

Kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Kenya kuingia awamu ya 22

0

Kinyang’anyiro cha taji la Ligi Kuu nchini Kenya FKF kitaingia raundi ya 22 mwishoni mwa Juma hili kati ya Februari 17 na 18.

Runinga ya Taifa KBC Channel 1 itarusha mubashara mechi mbili zitakazosakatwa katika uwanja wa Polisi Sacco,Posta Rangers wanaokalia nafasi ya tatu ligini wakiwa nyumbani dhidi ya wanajeshi Ulinzi Stars walio katika nafasi ya 11.

Baadaye saa kumi alasiri Shabana FC wanaokabiliwa na hatari ya kuenguliwa ligini watawazuru wenyeji Police FC katika uwanja wa Police Sacco.

Katika ratiba nyingine ya Jumamosi Murang’a Seal watakuwa nyumbani katika uwanja wa Sportpesa kuwatumbuiza Bidco United saa tisa, wakati Nzoia Sugar wakicheza nyumbani Sudi dhidi ya Bandari FC saa tisa, nao vinara wa ligi Gor Mahia wahitimishe ratiba ugenini katika uchanjaa wa kaunti ya Machakos dhidi ya wenyeji Nairobi City Stars kuanzia saa kumi alasiri.

Website | + posts