Kinyang’anyiro cha Ligi kuu Kenya kitarejea mwishoni mwa juma hili baada, ya mapumziko ya wiki mbili kupisha mechi za kimataifa na mechi za kombe la Mozart Bet.
Wagema mvinyo Tusker FC watafungua ratiba ugenini Jumamosi saa saba adhuhuri dhidi ya Kariobangi Sharks uwanjani Machakos,kabla ya mabingwa watetezi Gor Mahia kushuka ugani humo dhidi ya Kakamega Homeboyz saa kumi alasiri.
Mida ya saa tisa alasiri kesho,Shabana FC watakuwa nyumbani katika uwanja wa Raila Odinga dhidi ya Posta Rangers ,huku wenyeji Ulinzi Stars wakiwa nyumbani Ulinzi Sports Complex dhidi ya Posta Rangers .
Muhoroni Youth watakuwa nyumbani kesho saa tisa dhidi ya Nairobi City Stars .
Jumapili KCB watakuwa Machakos dhidi ya Bidco United kuanzia saa saba, na baadaye kuwapisha FC Talanta dhidi ya Police saa kumi alasiri,mechi zote zikirushwa mubashara na runinga ya KBC.
Murang’a Seal watakuwa nyumbani ugani Sport Pesa Arena saa tisa kuvaana na Nzoia Sugar wakati AFC Leopards wakishuka kiwarani Nyayo dhidi ya Sofapaka saa tisa alasiri.