Home Michezo Kindumbwendumbwe cha Sakaja Super Cup kuanza Jumamosi

Kindumbwendumbwe cha Sakaja Super Cup kuanza Jumamosi

0

Makala ya kwanza ya mashindano ya kuwania taji ya Sakaja Super Cup,yataanza rasmi Jumamosi Septemba 30 katika wodi zote 85 za kaunti ya Nairobi .

Mashindano hayo yanadhaminiwa na Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja.

Timu 340 zilizojiandikisha kushiriki zimetengwa katika makundi manne ya timu tano tano ,kutoka kila eneo bunge la kaunti ya Nairobi.

Kilele cha mashindano hayo ni Disemba 16 ambapo timu mshindi itatuzwa shilingi milioni 3,nambari mbili shilingi milioni na milioni 1 kwa timu ya tatu.

Gavana Sakaja anafadhili mashindano hayo kupitia kwa wakfu wake.

Website | + posts