Home Habari Kuu Kindiki: Tutachapisha majina ya majangili wote Lamu

Kindiki: Tutachapisha majina ya majangili wote Lamu

0
Waziri wa Usalama Prof. Kithure Kindiki.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki amesema kuwa wamebaini  na hivi karibuni watachapisha majina ya watu wote wanaojihusisha au kuwafadhili majangili sugu katika kaunti ya Lamu.

Waziri Kindiki amekariri kujitolea kwa serikali kutokomeza utovu wa usalama katika kaunti ya Lamu ambao umekuwa ukisababishwa na makundi haramu kama vile Al-Shabaab.

Ameongeza kuwa wale wote watakaokamatwa wataadhibiwa kisheria.

Website | + posts