Home Habari Kuu Kindiki: Serikali inaunda sera ya kuwaajiri wazee wa vijiji

Kindiki: Serikali inaunda sera ya kuwaajiri wazee wa vijiji

0

Serikali inaunda sera na mpangokazi wa kisheria wa kuwaajiri na kuwalipa mishahara wazee wa vijiji. Lengo ni kuangazia, miongoni  mwa mambo mengine, majukumu yao, masharti ya kuajiriwa, njia ya kuwaajiri, namna ya kuwafuta kazi, taratibu za nidhamu, masharti na taratibu za wao kuondoka ofisini.

Kulingana na Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki, wazee wa vijiji hutekeleza wajibu muhimu katika kukuza amani na mshikamano katika jamii.

“Wazee wa vijiji ni daraja kati ya serikali na raia na wanawezesha utekelezaji wa mipango ya serikali mashinani,” alisema Waziri wa Kindiki alipofika mbele ya Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mambo ya Kigeni ya bunge la Seneti leo Alhamisi.

Kindiki alifika mbele ya kamati hiyo kuangazia masuala ya kutambuliwa na kulipwa mishahara kwa wazee wa vijiji chini ya mpango wa Nyumba Kumi na wizi wa mifugo uliokithiri katika kaunti ya Kajiado.

Ili kukabiliana vilivyo na kuangamiza changamoto ya wizi wa mifugo, Waziri huyo alisema serikali itaendelea kupeleka vikosi vya usalama katika maeneo ambayo hukumbwa na wizi wa mifugo mara kwa mara, kuongeza uangalizi ili kufuatilia mifugo walioibwa na kuwakamata wahusika wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here