Home Habari Kuu Kindiki: Serikali haitabagua jamii yoyote katika vita dhidi ya uhalifu

Kindiki: Serikali haitabagua jamii yoyote katika vita dhidi ya uhalifu

Waziri aliwaagiza maafisa wa asasi za usalama kuwalenga wahalifu binafsi.

0

Maeneo yaliyotajwa na serikali kuwa hatari katika kaunti za North Rift, yatasalia kuwa hivyo huku oparesheni ya maliza uhalifu ikiendelea.

Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki, alihakikisha kuwa serikali haitabagua jamii yoyote katika vita dhidi ya ujangili na wizi wa mifugo.

Waziri aliwaagiza maafisa wa asasi za usalama kuwalenga wahalifu binafsi.

“Serikali haitabagua jamii yoyote. Serikali kwa ushirikiano na wananchi wanapaswa kuwatambua wahalifu wanao wahangaisha wakazi, na kuharibu taswira ya jamii nzima,” alisema Kindiki.

Kando na kurejesha mifugo walioibwa, Kindiki aliwaagiza maafisa wa usalama kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wafadhili wa wizi wa mifugo na wanaopatikana na mifugo walioibwa.

Waziri aliyasema hayo alipofungua rasmi kambi ya maafisa wa polisi wa kikosi cha GSU katika sehemu ya Akwichatis, kaunti ndogo ya Tiaty, kaunti ya Baringo,

Waziri alikuwa ameandamana na kamanda wa GSU Eliud Lagat, mbunge wa Tiaty William Kamket pamoja na maafisa wa serikali ya kitaifa na wale wa serikali ya kaunti ya baringo.

Website | + posts