Home Habari Kuu Kindiki asisitiza uhamisho wa polisi

Kindiki asisitiza uhamisho wa polisi

0

Waziri wa usalama wa taifa Profesa Kithure Kindiki, amesema kuwa uhamishimo wa maafisa wa usalama ni lazima na unaendelea kote nchini. Haya yanajiri wakati vita dhidi ya pombe na dawa haramu vimepamba moto.

Akizungumza mjini Nakuru alipotembelea vitengo vya usalama, kindiki alisema kuwa maafisa 42,500 ambao wamehudumu katika sehemu moja kwa muda mrefu, sasa watahamishwa.

Alisema hiyo ni njia moja ya kuboresha vita hivyo kwani baadhi ya maafisa na watumishi wengine wa umma walio na hamu na biashara hiyo haramu wanashukiwa kutatiza vita hivyo.

Vile vile, alimshukuru kamishina wa kaunti ya Nakuru Samuel Ndanyi kwa kukabili makundi ya magenge mjini humo.

Mwisho waziri alionya maafisa wa ardhi na wengine wanaojihusisha na ulagai wa ardhi ya umma kuwa, watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Boniface Musotsi
+ posts