Home Michezo Kinara wa soka Uhispania Luis Rubiales adinda kujiuzulu kutokana na busu

Kinara wa soka Uhispania Luis Rubiales adinda kujiuzulu kutokana na busu

0

Raisa wa shirikisho la kandnda nchini Uhispania RFEF Luis Rubiales, amekataa kata kata kujiuzulu kufuatia shutuma zinazomkabili baada ya kumbusu mchezaji wa timu ya taifa Jenni Hermoso katika shamrashamra za kusherehekea ushindi wa Kombe la Dunia.

Mapema wiki hii, Waziri Mkuu wa Uhispania alimtaka Ruabiales ajiuzulu kwa tendo hilo la fedheha akisema kuwa kuomba msamaha pekee hakutoshi.

Kinara huyo amesema kuwa busu hilo lilikuwa na makubaliano kati yake na mchezaji huyo na ni sawia na kumbusu mwanawe.

Rubiales awali pia alinaswa kwenye kamera akimshilikia mwanadada huyo kwenye kinena wakati wakisherehekea ushindi wa Kombe la Dunia walipoilaza Uingereza bao moja kwa sufuri.

Website | + posts