Home Habari Kuu Kimbunga cha Hidaya chatarajiwa pwani ya Kenya

Kimbunga cha Hidaya chatarajiwa pwani ya Kenya

0

Pwani ya Kenya inatarajiwa kukumbwa na kimbunga kijulikanacho kama Hidaya, mwishoni mwa juma hili huku serikali ikiwatahadhari wanaokaa karibu na bahari Hindi .

Kimbunga hicho pia kitaathiri pwani ya Tanzania na huenda kikasababisha madhara .

Haya yanajiri huku Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini ikionya kuhusu ongezeko la mvua katika maeneo kadhaa nchini.

Mkurugenzi wa idara hiyo David Gikungu ameonya kutokea kwa mafuriko zaidi katika maeneo yaliyo tambarare, na kuendelea kwa mvua ya masika hadi mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.

Serikali imetoa makataa ya saa 48 kwa wanaoishi umbali wa mita 30 kutoka kwa mito na maeneo yaliyo tambarare kuhamia maeneo salama.

Takriban watu 181 wameripotiwa kufariki kote nchini kutokana na athari za mafuriko ya mvua ya masika.

Website | + posts