Home Habari Kuu Kim Jong Un asimamia majaribio ya droni za vita

Kim Jong Un asimamia majaribio ya droni za vita

0
Kim Jong Un akifuatilia majaribio ya droni za kivita
kra

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesimamia majaribio ya droni za kivita zilizoundwa nchini humo. Haya ni kwa mujibu wa chumba cha habari kinachomilikiwa na serikali ya nchi hiyo KCNA.

Picha zilizochapishwa na chumba hicho cha habari zinaonyesha droni ya rangi nyeupe ikianguka kwenye kile kinachoonekana kama faru la kivita la Korea Kusini na kuliharibu.

kra

Kim, ambaye alikuwa ameketi akiwa amezungukwa na watu wanaoaminika kuwa washauri, amekuwa akiboresha zana za kivita za nchi yake huku mvutano ukishuhudiwa kati ya nchi hiyo na Marekani na Korea Kusini.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alisema kwamba mitindo ya ulimwengu katika majeshi imekuwa ni kuboresha zana za kivita za kiteknolojia ndiposa ameonelea aboreshe zana za jeshi lake.

Alihimiza wahusika kuimarisha utengenezaji wa zana mbali mbali zikiwemo droni zinazoweza kulipuka ambazo zitatumiwa na vitengo spesheli vya jeshi, zikiwemo droni zinazoweza kutumiwa hata kwenye maji.

Kim Jong Un alionekana mwenye furaha alipokuwa akifuatilia majaribio ya droni hizo.

Nchi hiyo imeboresha maradufu uwezo wake katika vita ambapo imekuwa ikijaribu makombora ya kina kifupi na ya kina kirefu ikilenga Korea Kusini huku ikikosa kutilia maanani vikwazo vya kimataifa kuhusiana na silaha.

Majaribio ya droni za kivita yanajiri baada ya wanajeshi wa Korea Kusini na wa Marekani kufanya mazoezi ya pamoja ili kuongeza uwezo wao wa pamoja kujilinda dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.

Inaripotiwa kwamba majaribio hayo yataendelea hadi Alhamisi.

Website | + posts