Home Habari Kuu Kikao cha kusikiliza mashtaka dhidi ya Gavana Mwangaza chaingia siku ya pili

Kikao cha kusikiliza mashtaka dhidi ya Gavana Mwangaza chaingia siku ya pili

0

Kikao cha kusikiliza mashtaka dhidi ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, kimeingia siku ya pili Jumatano katika bunge la Seneti.

Siku ya Jumanne, Gavana Mwangaza alikanusha mashtaka saba yaliyowasilishwa dhidi yake na bunge la kaunti ya Meru.

Gavana huyo anakabiliwa na mashtaka ya utumizi mbaya wa rasilimali za kaunti, mapendeleo na madai na utovu maadili. Mashtaka mengine ni pamoja na dhulma, kuwadhalilisha viongozi wengine, kufanya uteuzi kinyume cha sheria na kujitwika mamlaka asiyokuwa nayo .

Katika mawasilisho yake tangulizi kwa niaba ya bunge la Kaunti ya Meru, wakili kiongozi Muthomi Thiankolu alisema Seneti linapaswa kuidhinisha kufurushwa kwa gavana huyo.

Hii ni mara ya pili kwa bunge la Seneti kuamua hatima ya Gavana Mwangaza baada ya bunge hilo kumnusuru awali.

Gavana Mwangaza amekuwa akikwaruzana na Wawakilishi Wadi wa kaunti ya Meru mara kwa mara, na juhudi za kuwapatanisha hazijazaa matunda.

Website | + posts