Home Kimataifa Kiir amtimua mkuu wa majeshi kwa hofu ya mapinduzi

Kiir amtimua mkuu wa majeshi kwa hofu ya mapinduzi

0

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amempiga kalamu mkuu wa majeshi Majak Akec Malok kwa hofu ya mapinduzi ya serikali.

Kiir amemteua Atem Malor kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Rais Kiir alirejea nyumbani Jumapili iliyopita kutoka kongamano la mataifa ya Afrika nchini Saudi Arabia, wakati fununu zilikuwa zimeenea katika taifa lake kuhusu njama ya kuipindua serikali yake.

Hata hivyo, jeshi la Sudan Defence Forces lilikanusha madai hayo.

Yamkini huenda Kiir akafanya mageuzi kadhaa serikalini ili kudhibiti hali.

Website | + posts