Home Biashara KICC kunadiwa kama kituo kinara cha mikutano na maonyesho

KICC kunadiwa kama kituo kinara cha mikutano na maonyesho

0

Jitihada zinafanywa ili kulinadi Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Kenyatta, KICC kama kituo bora cha kuandaa mikutano na maonyesho. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Utalii Dkt. Alfred Mutua alipokutana na usimamizi wa KICC ukiongozwa na mwenyekiti wake wa bodi Adelina Mwau.

Wakati mkutano huo, Dkt. Mutua alisema alitaarifiwa juu ya juhudi zinazofanywa kuvutia watalii kupitia uandaaji wa mikutano na maonyesho katika jumba hilo.

“Bodi ilitoa maelezo ya mikakati inayofanywa ili kubuni mpango mpya wa kuipigia debe KICC unaolenga kuinadi kama kituo kinara cha kuandaa mikutano na maonyesho katika kanda hii,” alisema Dkt. Mutua.