Home Michezo Kibiwott,Koech na Bett wafuzu kwa fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na...

Kibiwott,Koech na Bett wafuzu kwa fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji

0

Wanariadha wote watatu wa Kenya Leonard Bett,Abraham Kibiwott na  Simon Koech wamefuzu kwa fainali ya mbio za mita mita 3,000 kuruka viunzi na  katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha Ulimwenguni mjini Budapest Hungary Jumamosi Adhuhuri.

Bett amemaliza wa tatu katika mchujo wa tatu kwa dakika 8 sekunde 16 nukta 74,mchujo ulioshindwa na Lamecha Girma wa  Ethiopia.

Kibiwot lifuzu kwa fainali baada ya kuchukua nafasi ya nne katika mchujo wa pili  akitumia dakika 8 sekunde 24 nukta  nukta 31, katika mchujo ulioongozwa na Kenth Rooks wa Marekani.

Koech alimaliza wa tatu katika mchujo wa kwanza kwa dakika sekunde 20 nukta 29  na kujikatia tiketi kwa fainali .

Fainali ya shindano hilo itaandaliwa Jumanne ijayo huku Wakenya hao wakipambana na bingwa mtetezi Soufiane El Bakkali wa Morocco.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here