Home Michezo Kibarua kigumu Simba waangukia Ahly tena,Yanga wapangwa na Mamelodi robo fainali Ligi...

Kibarua kigumu Simba waangukia Ahly tena,Yanga wapangwa na Mamelodi robo fainali Ligi ya Mabingwa

0

Miamba wa Tanzania klabu ya Simba wameratibiwa kumenyana tena na Al A hly ya Misri katika kwota fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku watani Yanga wakikumbana na Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini.

Simba walitoka sare na Ahly katika mechi zote za robo fainali kuwania kombe la AFL,na kwa jumla wamekutana mara tano kila moja ikishinda mbili na kuishia sare mara moja.

Kwenye droo iliyoandaliwa jijini Cairo Esperance kutoka Tunisia itakumbana na Asec Mimosas ya Ivory Coast, wakati miamba wa Angola Petro Atletico wakipangwa dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Duru ya kwanza ya robo fainali ipatapigwa Machi 29 huku marudio yakiwa April 5.

Website | + posts