Home Burudani KFCB kushirikiana na TikTok kuhamasisha umma kuhusu usalama mtandaoni

KFCB kushirikiana na TikTok kuhamasisha umma kuhusu usalama mtandaoni

0
kra

Usimamizi wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini KFCB umetangaza ujio wa kampeni ya uhamasisho kuhusu usalama mitandaoni itakayoandaliwa kwa ushirikiano na kampuni ya TikTok.

Hii ni baada ya kaimu mkurugenzi mtendaji wa KFCB Paskal Opiyo kukutana na wawakilishi wa kampuni ya TikTok wakiongozwa na Fortune Mgwili Sibanda anayesimamia mahusoiano na serikali na sera za umma katika eneo la Sub-Saharan Africa.

kra

Kampeni hiyo kwa jina “Safer Together” inalenga kuhakikisha usalama wa watoto mitandaoni hasa katika kuhakikisha kwamba hawatazami video za mada zisizohusu watoto.

Opiyo alipongeza maafisa hao kutoka TikTok kwa kuomba ushirikiano ambao alisema ni muhimu katika kudhibiti maudhui mitandaoni. Alisema KFCB na TikTok zina maono sawa hasa ulinzi wa watot mitandaoni.

Fortune kwa upande wake alisema kwamba wanafurahia kushirikiana na KFCB kutoa uhamasisho kwa umma wakilenga wazazi, walezi, wabunifu na wanafunzi.

Suala la maudhui ya moja kwa moja kwenye jukwaa la TikTok pia lilijadiliwa kwenye mkutano huo ambapo KFCB huenda ikahusishwa katika udhibiti ili kuhakikisha maudhui hayo yanawiana na kanuni zilizowekwa.

Awali KFCB na TikTok zilishirikiana katika masuala mbali mbali kama vile mpango wa kufahamisha wazazi kuhusu masuala ya kidijitali na wa kufahamisha vyombo vya habari kuhusu masuala ya kidijitali.

Website | + posts