Home Kimataifa Keter afika mbele ya DCI baada ya kukamatwa na kuachiliwa

Keter afika mbele ya DCI baada ya kukamatwa na kuachiliwa

0
kra

Aliyekuwa Mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter amefika mbele ya Idara ya uchunguzi wa kesi za jinai – DCI, mapema leo Jumatatu baada ya kukamatwa na kuachiliwa huru na polisi.

Keter alinaswa Jumapili mtaani Kileleshwa akitoka kwenye ibada na familia yake kutokana na kile kilichotajwa na DCI kuwa uchunguzi dhidi ya sakata ya ulangazi wa silaha na  kuchochea ghasia.

kra

Mbunge huyo wa zamani amefika kwenye makao makuu ya DCI leo Jumatatu akiandamana na mawakili wake.

Keter amekanusha tuhuma dhidi yake akisema zimechochewa kisiasa.

Website | + posts