Home Habari Kuu Kesi ya rufaa dhidi ya Joshua Waiganjo yafungwa

Kesi ya rufaa dhidi ya Joshua Waiganjo yafungwa

0

Jaji Grace Nzioka amefunga kesi ya rufaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuhusiana na polisi bandia Joshua Waiganjo.

Nzioka aliafikia uamuzi huo baada ya mahakama ya rufaa kutoa uamuzi ikisema kwamba agizo la mahakama kuu la kusikilizwa upya si sahihi au la kisheria katika mazingira hayo.

Jaji Nzioka alisema kuwa kesi hiyo imepitwa na wakati hivyo basi imefikia tamati yake.

“Suala hili limepitwa na wakati hivyo kufungwa,” mahakama ilibainisha.

Mahakama ya rufaa katika uamuzi wake ilisema kuwa mashtaka ya Waiganjo yatupiliwe mbali na aachiliwe huru.

Waiganjo alishtakiwa kuwa kati ya mwezi Juni na Disemba mwaka wa 2014, alijisingizia kuwa afisa wa polisi. Hata hivyo, aliachiliwa huru mwaka wa 2020.

Alphas Lagat
+ posts