Hukumu kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani iliyokuwa itolewe leo Ijumaa, imeahirishwa tena hadi tarehe 26 mwezi Januari mwaka 2024.
Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka, alidokeza kuwa hatua ya kuahirishwa kutolewa hukumu hiyo, ilisababishwa na kucheleweshwa kujumuishwa kwa ushahidi uliotajwa kuwa muhimu.
Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa washtakiwa katika kesi hiyo mwanahabari Jackie Maribe na Jowie Irungu, watasubiri zaidi kabla ya kujua hatima yao.
Wahusika wote wakiwemo wazazi wa washtakiwa walikuwa katika mahakama za Milimani, wakati habari za kuahirishwa kutolewa hukumu ya kesi hiyo zilipotolewa.
Aidha familia ya Monica Kimani ililezea kutoridhishwa kwao na hatua hiyo, ikisema inahujumu utoaji wa haki.