Home Habari Kuu Kesi dhidi ya Sudi ya kughushi vyeti vya masomo kurejelewa wiki hii

Kesi dhidi ya Sudi ya kughushi vyeti vya masomo kurejelewa wiki hii

Kesi dhidi ya Sudi ni miongoni mwa kesi nne ambazo zimeratibiwa kutajwa juma hili katika mahakama ya Milimani ya kukabiliana na ufisadi.

0
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi.

Kesi dhidi ya mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambapo anadaiwa kughushi vyeti vyake ya masomo itatajwa Jumanne wiki hii.

Mbunge huyo ameshtakiwa kwa kuwasilisha vyeti vya masomo ambavyo ni vya kughushi kwa tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.

Kesi dhidi ya Sudi ni miongoni mwa kesi nne ambazo zimeratibiwa kutajwa juma hili katika mahakama ya Milimani ya kukabiliana na ufisadi

Javason Kimemia Maina pia anakabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha mtihani wa kidato cha nne, KCSE kutoka shule ya upili ya Kimuri, alichotumia kuajiriwa katika Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi nchini, EACC.

“Anashtakiwa kwa kupokea fedha za umma kinyume cha sheria, kughushi na kuwasilisha stakabadhi bandia. Madai hayo yanahusishwa na kughushi stakabadhi ili kupata ajira,” ilisema EACC kupitia ukurasa wake wa X.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo serikali imeimarisha msako dhidi watumishi wa umma ambao walitumia vyeti ghushi vya masomo kupata ajira katika utumishi wa umma.

Kesi zingine ni pamoja na ile ya mkurugenzi wa kampuni ya GDC Silas Masinde na wengine wanane, ambayo itasikizwa tarehe tano mwezi Aprili.