Home Habari Kuu Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa fainali za kombe la bara Afrika mwaka...

Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa fainali za kombe la bara Afrika mwaka 2027

Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe, alitoa tangazo hilo siku ya Jumatano Jijini Cairo Misri.

0
Kenya kuandaa finali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2027.

Kenya, Tanzania na  Uganda zitaandaa fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2027.

Tangazo hilo lilitolewa leo Jumatano jijini Cairo nchini Misri, huku ombi la pamoja la mataifa ya Afrika Mashariki likipiku lile la Misri, Botswana na Algeria ambazo zilijiondoa katika kinyangányiro hicho.

Tangazo hilo lilitolewa na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe.

Mataifa ya Afrika Mashariki yanahitaji angalau viwanja viwili kuandaa mashindano hayo pamoja na viwanja vingine vya mazoezi.

Algeria ilijiondoa katika kinyangányiro hicho siku ya mwisho kabla ya tangazo hilo, huku Misri, Senegal na Botswana zikijikaza hadi dakika za mwisho. Lakini juhudi zao hazikufua dafu pale mataifa ya Afrika Mashariki yalipotangazwa kuwa waandaaji wa fainali hizo.

Kenya imeorodhesha viwanja vya Nyayo, Kasarani na Kipchoge Keino, ilhali Uganda inanuia kuandaa fainali hizo katika viwanja vya Nelson Mandela, Nakivubo, Akii Bua na Hoima.

Tanzania itaandaa mechi hizo katika viwanja vya Benjamin Mkapa, Chamazi na CCM Kirumba.