Home Habari Kuu Kenya yawahamisha raia wake kutoka Israel

Kenya yawahamisha raia wake kutoka Israel

Kundi la kwanza la Wakenya 11 liliwasili jana Jumatano kulingana na Katibu katika Idara ya Masuala ya Mataifa ya Kigeni katika Wizara ya Mambo ya Nje, Roseline Njogu. 

0
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas katika eneo la Gaza.
kra

Kenya imeanzisha shughuli ya kuwahamisha raia wake kutoka Israel kufuatia kuzuka kwa vita kati ya taifa hilo la Mashariki ya Kati na kundi la Hamas siku 10 zilizopita.

Kundi la kwanza la Wakenya 11 liliwasili jana Jumatano kulingana na Katibu katika Idara ya Masuala ya Mataifa ya Kigeni katika Wizara ya Mambo ya Nje, Roseline Njogu.

kra

Kwa sasa, kuna zaidi ya raia 500 waliosajiliwa na ubalozi wa Kenya nchini Israel huku idadi kubwa wakiishi katika maeneo ambayo yamesalia salama na ambayo hayajaathiriwa na uhasama unaoendelea.

Mwanzoni mwa mzozo huo, baadhi ya raia wa Kenya waliamua kuondoka.

Wakenya nchini Israel kimsingi wanajumuisha wanafunzi, watu binafsi katika hija za kidini, au wale wanaofanya programu fupi za utafiti wa kisayansi.