Home Habari Kuu Kenya yatia saini Itifaki ya IGAD ya uhamishaji mifugo

Kenya yatia saini Itifaki ya IGAD ya uhamishaji mifugo

0

Kenya imetia saini rasmi itifaki ya IGAD juu ya uhamishaji mifugo, na kuwa nchi ya tano kuidhinisha makubaliano hayo yenye lengo la kudhibiti uhamishaji mifugo wa kuvuka mpaka ndani ya eneo hilo.

Utiaji saini huo ulifanywa na Waziri mwenye Mamlaka Makuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi wakati wa mkutano na wajumbe wa Sekretarieti wa IGAD wakiongozwa na Mkuu wa Ujumbe wa IGAD nchini Kenya Dk. Fatma Adan.

Itifaki hiyo iliyopitishwa wakati wa Kikao cha 72 na Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa IGAD mnamo Juni 24, 2021, itaweka mfumo wa usafirishaji huru, salama na wenye utaratibu wa mifugo na wafugaji wanaopitia katika nchi chini ya IGAD wakitafuta maji na malisho.

Hatua hiyo inalenga kuiwezesha IGAD kuzuia na kutatua migogoro, kustawisha kuishi kwa amani, na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi jirani ili kushughulikia changamoto za pamoja za kuvuka mpaka.

Hafla ya utiaji saini huo ilihudhuriwa na viongozi wakuu akiwemo Jonathan Mueke ambaye ni Katibu wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo, Kanali mstaafu Ali Raso Dido, Sarah Korere kutoka Kikundi cha Wafugaji wa Bunge, na Balozi Joseph Vungo ambaye ni Msajili wa Mikataba katika Idara ya Mambo ya Nje.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here