Home Habari Kuu Kenya yatafakari kuwaondolea raia wote wa dunia hitaji la viza

Kenya yatafakari kuwaondolea raia wote wa dunia hitaji la viza

0

Serikali ya Kenya inafikiria kuondoa hitaji la viza kwa watu wote wanaozuru taifa hilo. 

Hitaji hilo huenda likaondolewa ndani ya mwaka mmoja ujao.

Rais William Ruto anasema kaunti ya Turkana inayopatikana nchini Kenya ndio asili ya binadamu.

“Hiyo ndio sababu serikali ya Kenya inawazia uwezekano, katika kipindi cha siku chache zijazo au ndani ya mwaka mmoja ujao, wa kuwawezesha raia wa dunia kutoka kila pembe ya dunia kuitembelea Kenya bila hitaji la viza,” alisema Rais William Ruto wakati akiongoza Tamasha ya Utalii na Utamaduni ya Turkana katika Kituo cha Utamadunii cha Ekalees.

“Hii ni kwa sababu siyo haki kwa mtu yeyote kuulizwa viza wakati anarejea nyumbani,” aliongeza Rais Ruto wakati wa tamasha hiyo iliyopewa jina Tobong’u Lore ikiwa na maana ya karibu nyumbani.

Tayari serikali za Afrika Kusini, Jamhuri ya Dekomrasia ya Congo, DRC, Indonesia Comoros, Senegal, Eritrea, Msumbiji na Djibouti miongoni mwa zingine zimewaondolea raia wa Kenya wanaoingia katika nchi hizo hitaji la viza katika hatua ambayo pia imechukuliwa na Kenya.

Kenya imekuwa ikishinikiza mataifa ya bara la Afrika kuondoa hitaji la viza ili kuwawezesha raia wa bara hilo kutembeleana bila vikwazo.

 

 

 

Website | + posts