Home Kimataifa Kenya yarejea katika mashindano ya msururu wa raga duniani

Kenya yarejea katika mashindano ya msururu wa raga duniani

0
kra

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande – Shujaa, imerejea kwenye mashindano ya msururu  wa raga duniani baada ya kuwatitiga Ujerumani pointi 33-15, kwenye mechi ya mwisho ya  mchujo jijini Madrid, Uhispania Jumapili jioni.

Kenya iliongoza kipindi cha kwanza cha mechi hiyo iliyosakatwa katika uchanjaa wa Wanda Metropolitana  alama  12-10, Vincent Onyala na Chrisant Ojwang wakifunga try moja kil mmoja, huku Evans Mboya akifunga Conversion.

kra

John Okoth aliongeza try nyingine kipindi cha pili naye Omondi akufunga conversion, kisha George Ooro na Kevin Wekesa wakaongeza try moja kila mmoja huku Omondi akiongeza conversion nyingine.

Awali, Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Kevin Wambua iliwashinda Samoa pointi 19-12 siku ya Ijumaa, kabla ya kupigwa na Uhispania alama 12-10 na kisha wakainyofoa Chile pointi 36 -7 katika mechi za mchujo.

Kenya inarejea kwenye mashindano ya msururu wa dunia baada ya kushushwa daraja  mwaka mmoja uliopita.