Home Habari Kuu Kenya yapongeza Algeria kwa kupiga jeki sekta ya kilimo nchini

Kenya yapongeza Algeria kwa kupiga jeki sekta ya kilimo nchini

Kenya na Algeria zinashirikiana  kuleta mabadiliko  kwenye mpango wa kifedha ili kuhakikisha kuna usawa. 

0
Rais Ruto ashauriana na Rais wa Algeria Tebboune Amadjidnchini Italia.
kra

Rais William Ruto ameipongeza Algeria kwa kuisaidia sekta ya kilimo hasaa katika utoaji wa mbolea ya gharama nafuu.

Wakati huo huo Rais Ruto kupitia mtandao wa X, pia aliishukuru nchi hiyo kwa usaidizi wa kifedha kwenye mpango wa usalama unao-ongozwa na  umoja wa mataifa  nchini  Haiti.

kra

Rais Ruto aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa G7  na rais  Tebboune Amadjid wa Algeria, Jijini Apulia, nchini Italia.

Rais huyo wa Algeria  pia aliahidi  kusaidia  Kenya kwenye azma yake ya  kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa  muungano wa Afrika.

Kenya na Algeria zinashirikiana  kuleta mabadiliko  kwenye mpango wa kifedha ili kuhakikisha kuna usawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here