Timu ya taifa ya Kenya kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 23 maarufu kama Emerging Stars, imeambulia kichapo cha mabao mawili kwa nunge kutoka kwa visiwa vya Comoros katika kundi B Jumapili .
Affane Said Djambae alipachika magoli yote kwa Comoros kunako dakika za 34 na 49.
Kenya watarejea uwanjani Jumanne Julai 2 kwa mkwangurano wa mwisho dhidi ya Zimbabwe.
Kenya imezoa alama 3 baada ya kuwalaza Zambia katika mchuano wa ufunguzi mabao mawili bila jawabu.