Home Habari Kuu Kenya yapata idhini ya kuwapeleka maafisa wa polisi Haiti

Kenya yapata idhini ya kuwapeleka maafisa wa polisi Haiti

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha ujumbe huo kwa mwaka mmoja na mapitio baada ya miezi tisa.

0

Umoja wa Mataifa umeunga mkono pendekezo la Kenya la kuongoza kikosi cha kimataifa cha usalama nchini Haiti, kujibu ombi la waziri mkuu wa taifa hilo la Karibean la kusaidiwa kurejesha utulivu.

Haiti imekumbwa na ghasia za magenge kwa miongo kadhaa lakini wimbi la ukatili liliongezeka baada ya mauaji ya Julai 2021 ya Rais Jovenel Moïse.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “matumizi makubwa ya nguvu yanahitajika” ili kuwapokonya silaha magenge hayo na kurejesha utulivu.

Ikitoa idhini hiyo, azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha ujumbe huo kwa mwaka mmoja na mapitio baada ya miezi tisa.

Kikosi hicho kipya kitafanya operesheni za pamoja za usalama na kitakuwa na mamlaka ya kukamata watu kwa ushirikiano na polisi wa Haiti, kulingana na azimio hilo.

Pia italenga kuweka mazingira ya kufanya uchaguzi. Haiti haijafanya uchaguzi tangu 2016.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Haiti Jean Victor Geneus aliuita uamuzi huo “mwanga wa matumaini kwa watu ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.”

Website | + posts