Home Michezo Kenya yamaliza ya 6 michezo ya Jumuiya ya Madola kwa chipukizi

Kenya yamaliza ya 6 michezo ya Jumuiya ya Madola kwa chipukizi

0

Kenya imemaliza ya sita katika makala ya 7 ya michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Trinidad and Tobago.

Kenya imezoa jumla ya medali 9, dhahabu 5 na fedha 4 hususan baada ya kutwaa dhahabu 3 mapema leo Ijumaa.

 

Kelvin Kimutai amenyakua dhahabu ya mita 800 kwa kutumia muda wa dakika 1, sekunde 50 nukta 14 akifungua ukurasa wa nishani za siku.

Josephat Sang alinyakua dhahabu ya pili ya michezo hiyo kwenye fainali ya mita 3000 akifuatwa na Andrew Kiptoo aliyenyakua fedha.

Nancy Cherop alidhihirisha ubabe wake aliposhinda dhahabu ya mita 3000 ikiwa pia ni dhahabu ya pili michezoni baada ya kutwaa ushindi wa mbio za mita 1500.

Matokeo ya mwaka huu yalikuwa bora kuliko yale ya miaka minne iliyopita mjini Nsassau, Bahamas ambapo dhahabu 3 na fedha 1 zilinyakuliwa.

Titus Mwonga na na Janet Chepkemoi walishinda nishani ya fedha kila mmoja huku Andrew Kiptoo Alamisi akinyakua medali mbili za fedha.

Dhahabu zilitwaliwa na Nancy Cherop na Josephat Sang walioshinda medali mbili kila mmoja wakati Kelvin Kimutai akinyakua dhababu ya mita 800.

Australi ilitwaa ubingwa kwa nishani 64, dhahabu 26, fedha 17 na shaba 21 ikifuatwa na Uingereza kwa medali 49, dhahabu 16, fedha 23 na shaba 10, huku Scotland ikichukua nafasi ya tatu kwa dhahabu 12, fedha na shaba 5.

Afrika Kusini ilimaliza ya nne na ya kwanza Afrika kwa medali 20, dhahabu 7, fedha 6 na shaba 6.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here