Home Habari Kuu Kenya yajiunga na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Kenya yajiunga na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

0
Kenya kuadhimisha siku ya Mazingira duniani katika chuo kikuu cha Embu.

Kenya leo Jumatano inajiunga na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.

Siku hiyo huadhimishwa tarehe tano mwezi Mei kila mwaka.

Hapa nchini, itaadhimishwa katika Chuo Kikuu cha Embu na kuongozwa na Waziri wa Misitu na Mazingira Soipan Tuya.

Maudhui ya mwaka huu ni “urejeshaji wa ardhi iliyoharibiwa, kukomesha kuenea kwa jangwa na kujenga uwezo wa kustahimili ukame”.

Huku akiongoza sherehe hizo, Waziri Tuya pia atazindua zoezi la kurejesha sehemu chemichemi ya Kaimbuthu kwa kupanda miti na kuweka ua.

Waziri Tuya ataandamana na Katibu wa Idara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi Mhandisi Festus Ng’eno na mwenzake wa Misitu Gitonga Mugambi.

Kulingana na ripoti ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, UNEP, zaidi ya watu bilioni 4 wameathiriwa na uharibifu wa ardhi na kuenea kwa jangwa.

Website | + posts