Home Biashara Kenya yajiunga na benki ya uwekezaji ya Asia AIIB

Kenya yajiunga na benki ya uwekezaji ya Asia AIIB

Kenya sasa ni miongoni mwa nchi 13 ambazo zimejiunga rasmi na benki hiyo, huku ikilenga kunufaika na benki hiyo kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo.

0
Rais William Ruto na Rais wa benki ya uwekezaji ya Asia AIIB Jin Liqun.
kra

Kenya imejiunga rasmi na benki ya uwekezaji na ustawishaji miundombinu ya Asia (AIIB), baada ya  kulipa ada zote zinazohitajika kujiunga na benki hiyo.

Hayo yalitangazwa leo Jumanne na Rais William Ruto, alipozuru makao makuu ya benki hiyo Jijini Beijing Uchina, ambapo Kenya ilitia saini ya makubaliano.

kra

Kenya sasa ni miongoni mwa nchi 13 ambazo zimejiunga rasmi na benki hiyo, huku ikilenga kunufaika na benki hiyo kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo.

“Uanachama huo utaiwezesha Kenya kupata ufadhili kwa miradi ya miundo mbinu, juhudi za kukabiliana na tabia nchi, uunganishwaji, ushirikiano wa kikanda na teknolojia,” alisema Rais Ruto.

Benki hiyo inalenga kufadhili asilimia  50 ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kufikia mwaka 2025.

Rais Ruto anahudhuria kongomano la ushirikiano kati ya Uchina na Afrika (FOCAC),Jijini Uchina.

Website | + posts