Home Kimataifa Kenya yaipaua Uruguay na kusajili ushindi wa kwanza Olimpiki

Kenya yaipaua Uruguay na kusajili ushindi wa kwanza Olimpiki

0
kra

Timu ya raga ya Kenya, Shujaa iliibwaga Uruguay alama 19-14 kupitia muda wa ziada na kusajili ushindi wa kwanza katika michezo ya Olimpiki jijini Paris nchini Ufaransa jana Alhamisi usiku.

John Okeyo, Samuel Asati na  Patrick Odongo walifunga tries za Kenya huku Anthony Mboya akifunga conversion mbili.

kra

Kenya itarejea uwanjani kesho Jumamosi kwa mechi ya kuwania nafasi ya 9 na 10 dhidi ya Samoa.

Mchuano huo utakuwa marudio baada ya Samoa kuikung’uta Kenya pointi 26-0 katika kundi B.