Home Kimataifa Kenya yaibuka bora Afrika katika Michezo ya Olimpiki Paris

Kenya yaibuka bora Afrika katika Michezo ya Olimpiki Paris

0
kra

Kenya imeibuka bora barani Afrika katika makala ya 33 ya Michezo ya Olimpiki iliyokamilika Jumapili jijini Paris nchini Ufaransa.

Kenya imezoa jumla ya medali 11, dhahabu 4 fedha 2 na shaba 5, matokeo ambayo yanakaribia yale ya mwaka 2021 mjini Tokyo, Japani ilikozoa dhahabu 4 fedha 4 na shaba 2.

kra

Beatrice Chebet alinyakua dhahabu mbili katika mbio za mita 5,000 na 10,000 huku Faith Kipyegon akihifadhi dhahabu ya mita 1,500. Emmanuel Wanyonyi alishinda dhahabu ya mbio za mita 800.

Washindi wa medali za fedha walikuwa Ronald Kwemoi katika mita 5,000 na Faith Kipyegon katika mita 5,000.

Shaba zilitwaliwa na Mary Moraa katika mita 800, Benson Kipruto na Hellen Obiri katika marathoni, Faith Cherotich na Abraham Kibiwot katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Kenya iliwakilishwa na kikosi cha wanamichezo 124 katika raga ya wachezaji saba upande wanaume, voliboli wanawake, uogeleaji, Fencing, Judo na riadha.

Website | + posts