Home Michezo Kenya yaangushwa na Cameroon mashindano ya Voliboli Afrika

Kenya yaangushwa na Cameroon mashindano ya Voliboli Afrika

Timu ya taifa ya Voliboli ya wanaume ya Kenya maarufu kama Wafalme Stars ilianza vibaya mashindano ya kuwania kombe la bara Afrika walipotitigwa seti 3-1 na Cameroon,

0

Timu ya taifa ya voliboli ya wanaume ya Kenya maarufu kama Wafalme Stars ilianza vibaya mashindano ya kuwania kombe la bara Afrika walipotitigwa seti 3-1 na Cameroon jana Jumatatu usiku jijini Cairo, Misri.

Cameroon walitwaa seti mbili za mwanzo alama 25-22 na 25-20 kabla ya Kenya kujizatiti na kushinda seti ya tatu 26-24.

Hata hivyo, maji yalizidi unga kwa Kenya walipopoteza seti ya 25-17.

Website | + posts