Home Kimataifa Kenya yaangukia Cameroon,Namibia na Zimbabwe kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco

Kenya yaangukia Cameroon,Namibia na Zimbabwe kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco

0
Harambee Stars yafungana bao 1-1 na Burundi.
kra

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars imerushwa kundi J, katika safari ya kufuzu kwa kipute cha AFCON mwaka 2025 nchini Morocco.

Kulingana ba droo iliyoandaliwa Alhamisi jioni nchini Afrika Kusini, Stars imo kundi J pamoja na mabingwa mara tano Cameroon na waakilishi wa ukanda wa COSAFA Zimbabwe na Namibia.

kra

Kenya wataanza safari nyumbani kwa kuwaalika Zimbabwe,kabla ya kuizuru Namibia mwezi Septemba mwaka huu.

Oktoba mwaka huu Kenya itawazuru Cameroon na kuwaalika Indomitable Lions hao katika mchuano wa marudio.

Katika mechi mbili za mwisho Novemba mwaka huu ,Kenya watawaalika Namibia na hatimaye kuzuru Zimbabwe.

Makundi:

Group A: Tunisia, Madagascar, Comoros, Gambia

Group B: Morocco, Gabon,Central Africa Republic, Lesotho

Group C: Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana

Group D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda

Group E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia

Group F: Ghana, Angola, Sudan, Niger

Group G: Cote d’Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad

Group H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia

Group I: Mali, Mozambique, Guinea Bissau, Eswatini

Group J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe

Group K: South Africa, Uganda, Congo, South Sudan

Group L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi

Timu mbili bora kutoka kila kundi isipokuwa kundi B, zitafuzu kwa fainali za AFCON pamoja na timu moja ya kundi B.

Timu hizo 23 zitajiunga na wenyeji Morocco kwa makala ya 35 ya kipute cha AFCON, kati ya Disemba 21 mwaka ujao hadi Januari 18 mwaka 2026.